Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

BAADA YA KUWA KOCHA WA SIMBA KWA MECHI 1….MOROCCO AFICHUA MAZITO..’MAZINGIRA MAGUMU’…

  • 4
Scroll Down To Discover

Aliyekuwa KOCHA wa muda wa Simba, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema haikuwa rahisi kuvuka mechi ya raundi ya kwanza kwa timu hiyo, kwani ilikuwa inacheza kwenye mazingira magumu kutokana na maandalizi finyu, kila kitu kikiwa hakiko kwenye mfumo wake wa kawaida pia bila mashabiki wake iliyowazoea uwanjani.

Ikiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi, Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Gaborone United ya Botswana, katika mchezo mkali na mgumu, ambapo Wekundu wa Msimbazi walinufaika na ushindi wa bao 1-0 walioupata wiki moja iliyopita nchini Botswana, hivyo kutinga raundi inayofuata kwa ushindi wa mabao 2-1.

Morocco aliisifu Gaborone United kuwa ni moja kati ya timu bora, tishio, yenye wachezaji wanapambana na kujituma, lakini kwa bahati mbaya ilikutana na timu kubwa yenye wachezaji wazoefu.

Kocha huyo ameonesha kufurahia kuivusha Simba hatua inayofuata, akisema kitendo cha yeye kukubali kazi hiyo ilikuwa ni kujitoa muhanga kwani hakuna kocha yoyote ambaye angekubali hilo kutokana na mazingira yaliyokuwapo.

“Nilijitoa muhanga, hakuna kocha yoyote ambaye angekubali kuchukua timu hii katika mazingira kama haya, kuna watu walidhani mimi nitafeli, lakini mimi nilikuwa na imani, ndiyo maana nilikubali, nilijua ugumu wa kazi hii na kama ingeshindikana ingekuwaje, lakini kama nilivyotegemea nimefanikiwa, nimefurahi sana,” alisema Morocco, ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kuhusu kutocheza vyema, alisema imetokana na mambo mbalimbali, ikiwamo kutokuwa na muda wa mazoezi kutokana jinsi alivyoichukua timu.

Kocha huyo alikabidhiwa timu baada ya kuondoka kwa Kocha Mkuu, Fadlu Davids, ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu, Raja Casablaca ya Morocco.

“Malengo ilikuwa kuivusha Simba hatua hii, haikuwa mchezo, ni hatari sana, lakini tumefanikiwa kuvuka salama.

Moja ya kazi ngumu kwangu kwenye mpira wa miguu ilikuwa ni mechi hii, nilikuwa na siku chache tu za maandalizi, haikuwa rahisi kabisa, muda ulikuwa mchache ndiyo maana sikubadilisha vitu vingi, nimejaribu tu kuhakikisha tunavuka, namshukuru kocha Selemani Matola na niliowakuta wamenipa msaada, kusema kweli ni mechi ambayo tumecheza huku kila kitu kikiwa hakiko kwenye mfumo wake wa kawaida,” alisema kocha huyo.

Akiwazungumzia wapinzani wao, alisema ni moja ya timu bora ambayo isingekutana na Simba ingefika mbali sana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini pia amesema kama ‘Wekundu wa Msimbazi’ wamevuka kikwazo wakiwa kwenye mazungira hayo magumu, basi watafika mbali kwenye michuano hiyo kwani kila kitu kitakaa sawa muda si mrefu.

“Tumecheza na timu nzuri sana, ukiiona utaidharau, lakini ni timu bora na ngumu kweli, ina wachezaji wazuri, wanapambana, wanajituma, wanataka kushinda, halafu ukichanganya na kwamba walikuwa wanacheza na Simba, walikuwa wanataka kuonesha uwezo wao ili waonekane,” alisema.

Aliongeza kuwa kucheza bila mashabiki wake kulifanya wachezaji wawe na morali ya chini na kuwapa nguvu wapinzani wao.

“Kucheza bila mashabiki pia kuliwapa nguvu wapinzani wetu, kulipunguza pia morali yetu, nafikiri tungecheza na mashabiki tungeweza kushinda hata mabao manne,” alisema Morocco.

Mashabiki wa Simba walilazimika kuangalia mchezo huo kwenye Luninga kutokana na kufungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kwa kile kilichodaiwa kufanya vurugu kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita dhidi ya Al Masry ya Misri.

Baada ya kuvuka hatua hiyo, Simba inatarajiwa kucheza dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini, Oktoba 17, mwaka huu ambapo itakuwa ugenini, kabla ya kurudiana nchini, Oktoba 24.

The post BAADA YA KUWA KOCHA WA SIMBA KWA MECHI 1….MOROCCO AFICHUA MAZITO..’MAZINGIRA MAGUMU’… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post Shamra Shamra za CCM Zatikisa Boma Ng’ombe, Wananchi Wajaa Uwanjani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook