Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

ALAF Yazindua Mpango wa Siku Mbili wa Elimu ya Afya kwa Wafanyakazi

Afisa Mtendaji Mkuu ALAF Limited, Bibhu Nanda (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa uzinduzi wa zoezi la siku mbili la utoaji wa elimu na upimaji wa afya kiwandani hapo. Kampuni ya ALAF Limited, inayoongoza katika suluhisho mbalimbali za ujenzi, leo imezindua mpango wa siku mbili wa kuwaelimisha wafanyakazi kuhusu afya ikiwa ni moja wapo ya kipaumbele cha kampuni hiyo katika kujali afya na ustawi wa wafanyakazi wa kampuni hiyo. Daktari wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma kutoka Taasisi ya Kansa, Ocean Road, Dk. Kandali Samwel, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa uzinduzi wa zoezi la siku mbili la utoaji wa elimu na upimaji wa afya kiwandani hapo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo linalofanyika katika makao makuu ya ALAF jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi.Hawa Bayumi alisema mpango huo ni sehemu ya dhamira ya ALAF ya ustawi wa wafanyakazi na uwajibikaji wa kijamii wa kampuni hiyo. Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka Hospital ya Shree Hindu Mandal, Dk. Sadiq Dawood, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa uzinduzi wa zoezi la siku mbili la utoaji wa elimu na upimaji wa afya kiwandani hapo. Kwa mujibu wa Bi Bayumi, zoezi hilo ni la hiari na litazingatia upimaji wa Saratani ya Matiti, Saratani ya tezi dume na ile ya homa ya ini pamoja na chanjo ambapo alitoa rai kwa wafanyakazi kujitokeza ili kupima afya zao. “Mpango huu unalenga kuelimisha wafanyikazi juu ya umuhimu wa kupima afya ambao ni pamoja kugundua mapema na hivyo kuzuia athari zinazoweza kujitokeza mapema ili kila mtu aweze kuishi maisha mazuri na yenye afya bora”, alisema. Bayuni aliendelea kusema kuwa zoezi hilo ni bure kwa wafanyakazi wote na kwamba watumishi wote watapata muda wa kutosha wa kuwasiliana na kupata ushauri wa wataalam wa afya. Pia alibainisha kuwa zoezi hilo litakuwa ni endelevu ili kuhakikisha wafanyakazi wanajenga utamaduni wa kupima afya zao ili waendelee kuwa na afya bora nje na ndani ya kazi. “Wafanyakazi ni nguvu kazi muhimu kwa ajili ya kampuni yetu ndiyo maana uongozi umeona umuhimu wa kuandaa zoezi hili ili kila mfanyakazi aweze kujua hali yake ya kiafya ndani ya siku hizi mbili kwani afya nzuri ndiyo itawawezesha kuendelea na kazi vizuri”, alisema. Aliendelea kusema kuwa kampuni ya ALAF itaendelea kuweka kipaumbele chake katika maswala ya afya na ustawi wa wafanyakazi wake kama sehemu ya juhudi zake zinazolenga kuifanya kampuni iwe na matokeo chanya kwenye mipango yake ya kazi. ALAF Limited ni kampuni inayoongoza nchini Tanzania katika kuzalisha bidhaa kwa ajili ya shughuli za ujenzi zinazohusiana na maswala ya uezekaji wa paa kw akutumia bidhaa za chuma. Madaktari kutoka Taasisi ya Kansa ya Ocean Road na Hospitali ya Hindu Mandal  walifanya semina kadhaa na wafanyakazi kabla ya zoezi la upimaji na chanjo. Kampuni hii Ilianzishwa mwaka wa 1960 na imeendelea kuwa taasisi muhimu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo kupitia sekta ya ujenzi hapa nchini ambapo pia huzalisha bidhaa zingine ikiwemo koili na mabomba kwa ajili ya shughuli za ujenzi.

BAADA YA KUWA KOCHA WA SIMBA KWA MECHI 1….MOROCCO AFICHUA MAZITO..’MAZINGIRA MAGUMU’…

Aliyekuwa KOCHA wa muda wa Simba, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema haikuwa rahisi kuvuka mechi ya raundi ya kwanza kwa timu hiyo, kwani ilikuwa inacheza kwenye mazingira magumu kutokana na maandalizi finyu, kila kitu kikiwa hakiko kwenye mfumo wake wa kawaida pia bila mashabiki wake iliyowazoea uwanjani. Ikiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi, Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Gaborone United ya Botswana, katika mchezo mkali na mgumu, ambapo Wekundu wa Msimbazi walinufaika na ushindi wa bao 1-0 walioupata wiki moja iliyopita nchini Botswana, hivyo kutinga raundi inayofuata kwa ushindi wa mabao 2-1. Morocco aliisifu Gaborone United kuwa ni moja kati ya timu bora, tishio, yenye wachezaji wanapambana na kujituma, lakini kwa bahati mbaya ilikutana na timu kubwa yenye wachezaji wazoefu. Kocha huyo ameonesha kufurahia kuivusha Simba hatua inayofuata, akisema kitendo cha yeye kukubali kazi hiyo ilikuwa ni kujitoa muhanga kwani hakuna kocha yoyote ambaye angekubali hilo kutokana na mazingira yaliyokuwapo. “Nilijitoa muhanga, hakuna kocha yoyote ambaye angekubali kuchukua timu hii katika mazingira kama haya, kuna watu walidhani mimi nitafeli, lakini mimi nilikuwa na imani, ndiyo maana nilikubali, nilijua ugumu wa kazi hii na kama ingeshindikana ingekuwaje, lakini kama nilivyotegemea nimefanikiwa, nimefurahi sana,” alisema Morocco, ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Kuhusu kutocheza vyema, alisema imetokana na mambo mbalimbali, ikiwamo kutokuwa na muda wa mazoezi kutokana jinsi alivyoichukua timu. Kocha huyo alikabidhiwa timu baada ya kuondoka kwa Kocha Mkuu, Fadlu Davids, ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu, Raja Casablaca ya Morocco. “Malengo ilikuwa kuivusha Simba hatua hii, haikuwa mchezo, ni hatari sana, lakini tumefanikiwa kuvuka salama. Moja ya kazi ngumu kwangu kwenye mpira wa miguu ilikuwa ni mechi hii, nilikuwa na siku chache tu za maandalizi, haikuwa rahisi kabisa, muda ulikuwa mchache ndiyo maana sikubadilisha vitu vingi, nimejaribu tu kuhakikisha tunavuka, namshukuru kocha Selemani Matola na niliowakuta wamenipa msaada, kusema kweli ni mechi ambayo tumecheza huku kila kitu kikiwa hakiko kwenye mfumo wake wa kawaida,” alisema kocha huyo. Akiwazungumzia wapinzani wao, alisema ni moja ya timu bora ambayo isingekutana na Simba ingefika mbali sana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini pia amesema kama ‘Wekundu wa Msimbazi’ wamevuka kikwazo wakiwa kwenye mazungira hayo magumu, basi watafika mbali kwenye michuano hiyo kwani kila kitu kitakaa sawa muda si mrefu. “Tumecheza na timu nzuri sana, ukiiona utaidharau, lakini ni timu bora na ngumu kweli, ina wachezaji wazuri, wanapambana, wanajituma, wanataka kushinda, halafu ukichanganya na kwamba walikuwa wanacheza na Simba, walikuwa wanataka kuonesha uwezo wao ili waonekane,” alisema. Aliongeza kuwa kucheza bila mashabiki wake kulifanya wachezaji wawe na morali ya chini na kuwapa nguvu wapinzani wao. “Kucheza bila mashabiki pia kuliwapa nguvu wapinzani wetu, kulipunguza pia morali yetu, nafikiri tungecheza na mashabiki tungeweza kushinda hata mabao manne,” alisema Morocco. Mashabiki wa Simba walilazimika kuangalia mchezo huo kwenye Luninga kutokana na kufungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kwa kile kilichodaiwa kufanya vurugu kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita dhidi ya Al Masry ya Misri. Baada ya kuvuka hatua hiyo, Simba inatarajiwa kucheza dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini, Oktoba 17, mwaka huu ambapo itakuwa ugenini, kabla ya kurudiana nchini, Oktoba 24. The post BAADA YA KUWA KOCHA WA SIMBA KWA MECHI 1….MOROCCO AFICHUA MAZITO..’MAZINGIRA MAGUMU’… appeared first on Soka La Bongo.

BENKI YA NMB YAZINDUA TAWI MAALUM LA NMB TINDE  MNADANI

Na Mwandishi wetu, Shinyanga BENKI ya NMB imezindua tawi maalum la NMB Tinde Mnadani mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuzingatia dhamira yake ya muda mrefu ya kusambaza huduma za kifedha kwa jamii ambazo hazijafikiwa. Uzinduzi huu umeambatana pamoja na uzinduzi wa matawi mengine maalum ya Itobo(Nzega, Tabora), Iboregero(Igunga, Tabora), Mkongeni(Mvomero, Morogoro) na Dosidosi(Kiteto, Manyara) Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo ,Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi ameeleza kuwa Benki hiyo inatambua nafasi muhimu ya minada ya mifugo katika uchumi wa vijijini na uwepo wake katika mnada wa Tinde unaashiria utoaji wa huduma za kifedha na dhamira ya Benki ya NMB kusogeza huduma hizi kwa kila mtanzania huku wakiziwezesha jamii ambazo kihistoria zimekuwa zikikabiliwa na vikwazo vya kufikiwa na huduma za kifedha. Amesema eneo hilo la kimkakati la Tawi hili jipya maalum linalenga kuleta mapinduzi katika hali ya kifedha ya wafanyabiashara na wafugaji kwa kutoa huduma salama, rahisi na zenye ufanisi huku zikirahisisha na kuboresha shuguli zao kwa maslahi makubwa ya uchumi wa binafsi na wa mkoa wa Shinyanga kwa ujumla. “Kwa kuanzisha tawi hili maalum ndani ya mnada wa Tinde, tunatatua changamoto za moja kwa moja za matumizi makubwa ya pesa taslimu kwa kituo hiki kitatoa huduma kamili, zikiwemo kuweka pesa na kutoa pesa, kufanya miamala mbalimbali, programu za elimu ya kifedha hususani zeney mlengo wa ufugaji na mkopo maalum iliyoundwa kuongeza tija ya mifugo na biashara kwa ujumla, ” Mponzi alisema. Ameongeza kuwa, kabla ya hapo washiriki wa minada ya mifugo, wanunuzi na wafanyabiashara walilazimika kubeba pesa taslimu ili kuweza kufanya manunuzi au baada ya mauziano ya bidhaa. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Dk Kalekwa Kasanga “Uwekezaji huu wa Benki ya NMB utakuwa na faida kubwa kwa jamii yetu. Kwa kutoa njia salama na rahisi za kusimamia fedha, kupitia tawi hili maalum, uchumi wa Tinde utazidi kuimarika na watu wengi watanufaika zaidi na huduma hizi za kifedha na hivyo tutatengeza fursa za ajira na kuboresha hali ya jumla ya maisha kwa wakazi wetu.” Dk.Kasanga alisema. “Kwa upatikanaji wa mikopo na fursa ya kuweka akiba, wafugaji wataweza kuwekeza katika mifugo iliyoboreshwa, lishe bora na mbinu za kisasa za ufugaji, na hivyo kusababisha tija kubwa na kuongeza kipato. Hii pia itachochea mahitaji ya bidhaa na huduma nyingine, na kujenga mzunguko mzuri wa ukuaji wa uchumi,” aliongeza. Naye mfanyabiashara na mfugaji kutoka Tinde, Gerald Mwandu ameishukuru benki ya NMB kwa kujenga kituo hicho katika kata ya Tinde. Amewaomba wafugaji, wakulima na Wafanyabiashara kutumia huduma za benki mbalimbali za benki ya NMB.

Nafasi 24 za Ajira Serikalini

https://portal.ajira.go.tz/vacancies The post Nafasi 24 za Ajira Serikalini appeared first on SwahiliTimes.

ALAF Yazindua Mpango wa Siku Mbili wa Elimu ya Afya kwa Wafanyakazi

PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO OKTOBA 02 , 2025

BAADA YA KUWA KOCHA WA SIMBA KWA MECHI 1….MOROCCO AFICHUA MAZITO..’MAZINGIRA MAGUMU’…

BENKI YA NMB YAZINDUA TAWI MAALUM LA NMB TINDE  MNADANI

Nafasi 24 za Ajira Serikalini

Lastest News

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

Rais Mwinyi Ateua Wakurugenzi Wapya Serikalini

  • 13 Aug 2025
  • 107
© Image Copyrights Title

Brela Na Tmda Kushirikiana Katika Nyanja Ya Miliki Bunifu

  • 13 Aug 2025
  • 95
Read more News

Burudani

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

JENISTA MUHAGAMA AKIJUMUIKA NA WANA PERAMIHO

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 34
Read all News
© Image Copyrights Title

JENISTA MUHAGAMA AKIJUMUIKA NA WANA PERAMIHO

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 34
© Image Copyrights Title

USUSI WATAJWA KAMA FURSA YA AJIRA KWA VIJANA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 59
© Image Copyrights Title

GUMZO LA JIJI. KWA SASA NI AMARULA SUNDOWN SESSIONS

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 46
© Image Copyrights Title

MSANII BILL NASS ALIVYOWAIMBISHA WANANCHI KONDOA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 63
© Image Copyrights Title

WAZIRI DKT. GWAJIMA AMWAKILISHA SPIKA WA BUNGE DKT. TULIA AKSON KWENYE HAFLA YA MISS UNIVERSE TANZANIA, 2025,

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 74
© Image Copyrights Title

WAZIRI MWITA AWATAKA WANAMITINDO KUIWAKILISHA VEMA NCHI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 109
© Image Copyrights Title

“KAMA WAO” YAINGIA MTAANI! MUGGA MO NA BANDO MC WAPIGA KAZI SAFI

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 213
© Image Copyrights Title

ADONIJAH OWIRIWA ,  MTAYARISHAJI MKUU WA FESTAC ’77, ANASEMA

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 83
© Image Copyrights Title

BASATA YA WAJENGEA UELEWA WA MIFUMO KUSOMANA MAAFIA UTAMADUNI NA BIASHARA MARA 

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 79
© Image Copyrights Title

MAJALIWA: SANAA INAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA UCHUMI

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 77

Michezo

Don't miss daily news

© Image Copyrights Title

BAADA YA KUWA KOCHA WA SIMBA KWA MECHI 1….MOROCCO AFICHUA MAZITO..’MAZINGIRA MAGUMU’…

Lorem ipsum dosectetur adipisicing elit, sed do.Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur Nulla fringilla purus at leo dignissim congue. Mauris elementum accumsan leo vel tempor.

  • 16
Read all News
© Image Copyrights Title

BAADA YA KUWA KOCHA WA SIMBA KWA MECHI 1….MOROCCO AFICHUA MAZITO..’MAZINGIRA MAGUMU’…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 16
© Image Copyrights Title

MRITHI WA FADLU SIMBA HUYU HAPA….KOCHA WA MAN UNITED ATAJWA….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 30
© Image Copyrights Title

KISA NAMBA YA KUCHEZA… ‘TSHABALALA’ KASHALIANZISHA KWA BOKA HUKO YANGA…ISHU YAKE HII HAPA..

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 26
© Image Copyrights Title

KUHUSU SOKA ‘MAKANDE’ LA FOLZ ….TAMKO LA MABOSI YANGA HILI HAPA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 25
© Image Copyrights Title

RASMI…..FADLU ATOA YA MOYONI KUSEPA SIMBA….ATAJA VIONGOZI…ISHU YA FEI TOTO…..

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 22
© Image Copyrights Title

HIZI HAPA TAMU & CHUNGU ZA FADLU NDANI YA SIKU 444 ZA FADLU AKIWA NA SIMBA…

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 30
© Image Copyrights Title

BAADA YA KUANZA KINYONGE CAF….WASAUZI WA SIMBA WAFUNGUKA YA MOYONI….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 26
© Image Copyrights Title

KOCHA YANGA AMTAJA ALIYEIOKOA SIMBA NA KIPIGO CHA AIBU JUZI….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 53
© Image Copyrights Title

KWA HALI HII…YANGA WANAKAZI YA KUFANYA ANGOLA LEO…WAKIKAA VIBAYA TU CHALII….

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 49
© Image Copyrights Title

FURAHA YA KIPIGO CHA SIMBA YAZIMWA GHAFLA YANGA…..FOLZ AWAPA ‘KIJEMBE’ MASTAA..

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt .

  • 40
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook