Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Air Tanzania yatangaza ajira mpya 173

  • 6
Scroll Down To Discover

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limetangaza nafasi 173 za ajira, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulipanua na kulipa nguvu zaidi shirika hilo ndani na nje ya Afrika.

ATCL, inayomilikiwa na Serikali, inatafuta marubani wapya, wahudumu wa ndege na wafanyakazi wa ardhini, ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Mkakati wa Miaka Mitano. Mpango huo unalenga kupanua njia za safari na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha muongo uliopita.

Kulingana na tangazo hilo, nafasi zilizopo ni pamoja na marubani wakuu 23, marubani wasaidizi 45, wahudumu wa ndege 100 (ikiwemo 20 wenye ujuzi wa lugha ya Kifaransa na Kichina), mhasibu mmoja na wasaidizi wa mizigo 4.

Aidha, Shirika hilo limetangaza mwisho wa kutuma maombi hayo ni Oktoba 14, mwaka huu.

Ajira hizo zinakuja wakati ATCL ikiendelea kupanua huduma zake za kimataifa, ambapo tayari inafanya safari za ndege kwenda Guangzhou (China), Mumbai (India), Dubai (UAE), pamoja na mtandao wa safari za kikanda na za ndani.

The post Air Tanzania yatangaza ajira mpya 173 appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Dkt. Nchimbi Awasili Mtwara Kuendelea Kusaka Kura za Kishindo za Dkt. Samia
Next Post Serikali Yapinga Ripoti ya Human Rights Watch, Yaitaja Kujaa Upotoshaji
Related Posts
© Image Copyrights Title

Nafasi 24 za Ajira Serikalini

© Image Copyrights Title

Nafsi 23 za Ajira Serikalini

Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook