Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Nchimbi Awahimiza Wafanyabiashara wa Machinga Complex Kumpigia Kura Dkt. Samia

  • 2
Scroll Down To Discover

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia na kuzungumza na Wananchi wa Ilala-Machinga Complex leo Oktoba 01, 2025 akiendelea na mikutano yake ya kampeni kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mara baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala Ndugu Mussa Azzan Zungu pamoja na Madiwani .

Pamoja na hayo Dkt.Nchimbi amewahamiza Wananchi hao kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29,2025 na kumpigia kura za kutosha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Mdiwani na hatimae kuibuka na ushindi wa Kishindo.

Dkt. Nchimbi anahitimisha kampeni zake leo kwa mkoa wa Dar es Salaam akifikisha mkoa wa 15 tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar na kuelekea mikoa mingine kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 



Prev Post Kampuni ya Network Yashirikiana na Flydubai Kuzindua Malipo ya Simu kwa Wateja
Next Post Dkt.Nchimbi Awanadi Wabunge wa Mkoa wa Dar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook