Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia Acheza Taarab na Mama Karume Katika Mkutano wa Kampeni Tanga – Video

  • 9
Scroll Down To Discover

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akicheza mziki wa Taarab na Mama Fatma Karume, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM uliofanyika Tanga mjini, tarehe 29 Septemba, 2025.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuvuta hisia za maelfu ya wananchi baada ya kujumuika na kushiriki kucheza muziki wa taarab pamoja na Mama Fatma Karume, mjane wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.

Tukio hilo lililowapendeza mashabiki wengi lilifanyika tarehe 29 Septemba, 2025, katika mkutano mkubwa wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika mjini Tanga.

Wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani walilipuka kwa shangwe na vifijo walipowaona viongozi hao wakishiriki kwa furaha kucheza muziki wa taarab, jambo lililoonyesha mshikamano wa kiutamaduni na kijamii ndani ya chama hicho kikongwe.

Akihutubia wananchi, Dkt. Samia alisisitiza dhamira ya CCM kuendeleza amani, mshikamano na maendeleo ya Watanzania, huku akiwataka wananchi waendelee kuwa na imani na chama hicho katika kuwaletea maendeleo endelevu.

Aidha, alisema kampeni zake zimejikita katika kutatua changamoto za wananchi na kuongeza kasi ya miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea kote nchini, hususan katika sekta za elimu, afya, kilimo na miundombinu.

Kwa upande wake, Mama Fatma Karume alipongeza dhamira ya Dkt. Samia kuendeleza mshikamano wa kitaifa, huku akiwataka wanawake na vijana kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuijenga Tanzania yenye mshikimano na ustawi wa wote.

Mkutano huo wa Tanga ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, wagombea ubunge na udiwani, pamoja na maelfu ya wananchi waliokuwa na hamasa kubwa ya kushiriki kampeni hizo.



Prev Post Museveni VS Bobi kampeini za uchaguzi mkuu zaanza rasmi Uganda, katika Dira ya Dunia TV
Next Post Dk.Mwinyi Aahidi Kujenga Masoko Mapya 5 Zanzibar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook